Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 4:00 am

NEWS : RAIS WA SUDAN ATANGAZA HALI YA HATARI YA MIEZI SITA KATIKA MAJIMBO MAWILI

Rais wa Sudan atangaza hali ya hatari ya miezi sita katika majimbo mawili

Rais wa Sudan atangaza hali ya hatari ya miezi sita katika majimbo mawili

Rais Omar al Bashir wa Sudan ametangaza hali ya hatari ya miezi sita katika majimbo mawili ya nchi hiyo. Jana Jumamosi Rais al Bashir alitangaza uamuzi huo wa kutekelezwa hali ya hatari huko Kordofan ya Kaskazini na Kasala.

Dikrii hiyo inahitaji kuidhinishwa na bunge katika muda wa wiki mbili kabla ya kuanza kutekelezwa. Duru za habari nchini Sudan zimearifu kuwa hatua hiyo ni sehemu ya kampeni za upokonyaji silaha zinazoendelea karibu na jimbo la Darfur na huko Blue Nile. Itafahamika kuwa hali ya hatari tayari inatekelezwa katika mikoa mingine saba iliyokumbwa na machafuko huko Sudan ambayo inaunda jimbo la Darfur ambako vikosi vya serikali vimekuwa vikipambana na wanamgambo wenye silaha tangu mwaka 2003.

Watu zaidi ya milioni 2.5 wamelazimika kuyahama makazi yao na wengine 300,000 wameuawa tangu kujiri machafuko katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan 2003.