Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 2:27 am

NEWS : RAIS WA MISRI ASISITIZA KUTOGOMBEA TENA UCHAGUZI UJAO

Rais Al-Sisi wa Misri: Ninaheshimu katiba, sitagombea uchaguzi wa mwakani

Rais Al-Sisi wa Misri: Ninaheshimu katiba, sitagombea uchaguzi wa mwakani

Rais Abdel Fattah el-Sisi wa Misri amesema kuwa, hatojiandikisha kwa jili ya kugombea tena ushaguzi wa rais ujao kwa muhula wa tatu.

Al-Sisi amesema kuwa, anaheshimu katiba ya Misri kuhusiana na suala la ukomo wa mihula miwili ya rais na kwa ajili hiyo hatoshiriki tena kugombea uchaguzi ujao. Ameongeza kuwa, kumetokea matukio makubwa nchini Misri hivyo bila matakwa ya Wamisri wenyewe, hawezi kugombea kipindi kingine cha tatu.

Rais Abdel Fattah el-Sisi wa Misri

Matamshi ya el-Sisi ambaye anakosolewa kwa ukandamizaji na ukiukaji wa haki za binaadamu, yametolewa katika hali ambayo Mohammed al-Swedi, kiongozi wa muungano wa wawakilishi wanaomuunga mkono rais huyo wa Misri unaoitwa 'Da'am Misr' siku chache zilizopita alinukuliwa akisema kuwa, hivi karibuni muungano huo utaanzisha kampeni ya wananchi kumtaka Rais Abdel Fattah el-Sisi agombee tena katika uchaguzi wa mwaka 2018. Muungano wa Da'am Misr unawajumuisha wabunge 317 wanaomuunga mkono rais wa nchi hiyo kati ya 596 wa bunge lote la Misri.