Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 11:48 am

NEWS: RAIS WA KOREA KASKAZINI KIM AMTEMBELEA RAIS WA CHINA XI JINPING

Tokeo la picha la kim travel to china today

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, ameanza ziara nchini China kwa mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Xi Jinping.

Rais Kim ameongozana na mke wake Ri Sol-ju na atakuwa nchini China hadi Januari 10.

Tokeo la picha la kim visit to china today

Ziara hiyo inaonesha kuwa kupanga mkutano wa pili kati ya rais Kim Jong un na rais wa Marekani Donald Trump zikiendelea.

Wawili hao walikutana mwezi Juni mwaka uliyopita hatua ambayo ilikuwa ni ya kwanza kwa rais wa Marekani aliye madarakani.

Siku ya Jumatano kulikuwa na madai kuwa bwana Kim huenda akatumia trani yake maalum kusafiri hadi China.

Tokeo la picha la kim visit to china today

Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini ambaye pia anaandamana na maafisa wake kadhaa, anazuru Uchina kwa mara ya nne katika kipindi cha chini ya mwaka mmoja.

Jumanne inaripotiwa kuwa siku ya kuzaliwa kwa kiongozi huyo ambaye anasherehekea miaka 35 ya siku yake ya kuzaliwa japo tarehe ya siku hiyo haijathibitishwa na Pyongyang.

China ni mshirika muhimu wa kidoplomasia wa Korea Kaskazini na moja ya vyanzo vikuu vya biashara na misaada.

"[Bwana] Kim anapania kuukumbusha utawala wa Tramp kwamba taifa lake lina njia mbadala ya kujikimu kiuchumi tofauti na ile inayotolewa na Washington na Seoul," Harry J Kazianis, mkurugenzi wa taasisi ya masomo ya ulinzi aliiambia shirika la habari la Reuters.