Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 6:43 am

NEWS: RAIS TRUMP AMUANDIKIA BARUA KIM JONG-UN YA KUSITISHA MKUTANO WAO

Rais wa Marekani Donald Trump amemuandikia Barua Rais wa Korea Kaskazin Kim Jong Un kusitisha mkutano wa kihistoria kati yake na kiongozi huyo uoliopangwa kufanyika mwezi ujao.

Amesema uamuzi wake umetokana na "ghadhabu kuu na ukali wa wazi" uliokuwa kwenye taarifa ya karibuni ya Korea Kaskazini.

Bw Trump amesema haingekuwa vyema kuendelea na mkutano huo nchini Singapore Juni 12 kama ilivyokuwa imepangwa.

Kwenye barua kwa Bw Kim, amesema anasubiri sana kwa hamu kukutana naye "siku moja".

Afisa wa cheo cha juu wa Korea Kaskazini alikuwa mapema leo amemlaumu Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence kwa kuwa "mjinga" na kuonya kuwa kutakuwa na maonyeshano ya ubabe wa nyuklia ikiwa mazungumzo yatafeli.

Choe Son-hui alisema Pyongyang haitaweza kuibembeleza Marekani kwa mazungumzo.

Siku za hivi karibuni pande hizo mbili zilikuwa zimeonya kuwa mkutano wa Juni 12 unaweza kuharishwa au kufutwa kabisa.

Korea Kaskazini ilisema itafikiria tena iwapo itahudhuria mkutano ikiwa Marekani itaendelea kusisitiza kuwa iachane na mpango wa silaha za nyuklia.

Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumanne alisema Korea Kaskazini ndiyo ingetimiza masharti ya kufanyika kwa mazungumzo hayo.

Choe Son-hui amehusika kwenye mazungumzo mara kadha na Marekani kwa karibu miaka kumi iliyopita.