- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MUGABE HATARINI KUPINDULIWA
Harare: Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe yupo kwenye hatari ya kupinduliwa kufuatia Jana Jeshi la Polisi Nchini humo kuvamia kitoa cha habari cha kitaifa ZBC.
Mapema leo Jumatano asubuhi Novemba 15 kwenye televisheni ya taifa, maafisa wa juu katika jeshi la nchi hiyo wamekanusha kuepo na mapinduzi ya kieshi.
Hali hii ilianza mapema alfajiri. hali ya kutia wasiwasi inakuja pale ambapo kulisikika milipuko kadhaa katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare, na askari wamedhibiti kiuo cha habari cha taifa ZBC. Hali ya sintofahamu inaendelea nchini humo.
Jana kwenye majira ya Saa 10:00 afajiri,katika tangazo lililorushwa kwenye televisheni ya taifa, jeshi lilikanusha kuepo kwa mapinduzi ya kijeshi nchini Zimbabwe. Sio "mapinduzi ya kijeshi", jeshi liliongea.
Jeshi lilisema kwamba Robert Mugabe na familia yake wako salama. Muda mfupi kabla, shirika la habari la AFP, likimnukuu shahidi mmoja, lilisema kuwa ilisikika milipuko karibu na makazi binafsi ya rais Mugabe. "Tunalenga wahalifu walio karibu naye ... wakati lengo letu litakamilika, tunatarajia kurejea kwa hali ya kawaida," afisa mmoja wa ngazi ya juu katika jeshi alisema.
Kamanda mkuu wa jeshi la Zimbabwe alionya kuingilia kati iwapo pande pinzani zitaendelea kuzozana ndani ya chama tawala cha Zanu-PF.Katika taarifa isio ya kawaida , Jenerali Constantino Chiwenga alitaka kusitishwa kwa vita dhidi ya wanachama waliopigania uhuru wa taifa hilo.
Matamshi yake yanajiri baada ya rais Robert Mugabe kumfuta kazi makamu wake wa rais aliyetarajiwa kumrithi Emmerson Mnangagwa.