Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 5:46 am

NEWS: RAIS MAGUFULI NA MUSEVEN WALAANI UWAMUZI WA ICC

Rais Magufuli amelaani hatua zilizochukuliwa na mahakama ya kihalifu ya ICC ambayo imemuagiza mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo kuanzisha uchunguzi dhidi ya mgogoro wa BurundI,Rais Magufuliamesema kuwa kitenndo hicho kinarudisha nyuma hatua zilizochukuliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo iliunda Kamati ya usuluhishi wa mgogoro wa Burundi inayoongozwa na Mhe. Rais Museveni na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa.

Mhe. Rais Magufuli amesema hali ya Burundi sio mbaya kama inavyotangazwa kwa kuwa tayari wakimbizi wengi waliokuwa Tanzania wamerejea Burundi na wengine wanaendelea kurejea, na pia viongozi wanaosuluhisha mgogoro huo wamepanga kukutana tarehe 23 Novemba, 2017 kwa lengo kuendeleza mchakato wa kutatua mgogoro huo.

Naye kwa upande wake Rais Museveni ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki amesema ICC inaingilia mambo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki bila kuwahusisha viongozi wa Jumuiya hiyo jambo ambalo sio sahihi na linarudisha nyuma juhudi za kutafuta amani ya nchini Burundi.

Rais Magufuli amemaliza ziara rasmi ya kiserikali ya siku 3 nchini Uganda na kurejea nchini Tanzania jana tarehe 11.11.2017

Mhe. Rais Magufuli ameagana na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika Mji wa Masaka na baadaye kusindikizwa na Makamu wa Rais wa Uganda Mhe. Edward Kiwanuka Sekandi hadi Mutukula, mpakani mwa Tanzania na Uganda.