- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI AWATAKA POLISI KUANZISHA VIWANDA ILI WAJITEGEMEE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli ameyataka majeshi yote ya polisi kushiriki katika shuguli za kiuchumi kwa kuanzisha viwanda ili waweze kujiendesha wenyewe.
“Ninataka muelekeo mpya wa majeshi yetu unaolenga kujenga uchumi wa kisasa, barabara nyingi kwa mfano kwenye Umoja wa Afrika zimejengwa na wanajeshi. Ninafahamu suala la sare za maaskari ni tatizo, ninataka nikiwaona askari wangu wawe wanapendeza hakuna ubaya kuwa na kiwanda kwani kitasaidia ninyi kujiendesha wenyewe,” alisisitiza Rais Magufuli
Rais Magufuli pia amewataka viongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani kushugulikia kero ndogo ndogo wanazokutana nazo askari katika mazingira yao ya kazi.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Desemba 21, 2018 katika hafla ya kuwatunuku vyeo maafisa na wakaguzi wasaidizi wa polisi iliyofanyika Kurasini Jijini Dar es salaam.
“Viongozi wa Wizara wa Mambo ya Ndani shughulikieni mambo madogo madogo, nimesikia wapo askari ambao wanahamishwa lakini hawalipwi fedha za uhamisho wakati kuna wengine wanalipwa,” amesema
Aliongeza kuwa, “Kero ndogondogo zinawavunja moyo polisi, kwani wapo askari wanakamata wahalifu halafu wanapigiwa simu na ofisa wawaachie wakati wao wanatimiza wajibu wao,”