- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI AWAONYA WANACCM.
DODOMA: Rais Wa Jamhuri ya muungano Dk John Pombe Magufuli amewataka wana_CCM kuchangua viongozi waadilifu, wachapa kazi na wenye maadili kwa nia ya kuleta maendeleo kwa Taifa.
Ameyasema hayo wakati akifungua mkutano mkuu Wa tisa Wa CCM uliofanyika leo mjini Dodoma.
Magufuli amesema ili Taifa kuwa na maendeleo mazuri ni lazima kama wana_CCM kuvunja makundi yaliyoanzishwa kipindi cha uchanguzi na matokeo uchanguzi umekwisha sasa ni wakati wa kuvunja makundi hayo kwa lengo la kuchapa kazi.
Pia amewataka wana_ CCM kuendelea kuwa wana_CCM wema ili kuleta manufaa na maendeleo ya nchi yetu.
Hata hivyo amewataka viongozi kutowaogopa watendaji Wa serikali katika masuala ya kupinga na kutetea Haki za wananchi katika harakati za kuleta maendeleo.
"Naomba ninukuu maneno ya mwalimu Nyerere aliyoyasema Juni 1968 kazi ya Chama kilicho imara ni kuunganisha wananchi na serikali kwa kuwaondoa na umasikini wao," amesema Magufuli.
Aidha ameongeza kwa kusema Chama kimedhamiria kupambana na rushwa na hakita sita kumchukulia hatua Mtu yoyote atakayetoa rushwa ili kupita kwenye uchanguzi.
Mbali na hayo amesema serikali imepanga katika harakati ya kufikia uchumi Wa kati na waviwanda na kudai kuwa mpaka sasa Viwanda 3306 tayari vimejengwa.
Pamoja na hayo amesema takribani jumla ya fedha za kigeni 5824 zimeongezeka .