- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI AWAJIBU WABUNGE NAPE NA BASHE SAKATA LA SGR
Dodoma: Rais John Pombe Magufuli amewataka wabunge wawili kutoka CCM Mbunge wa Mtama Nape Moses Nnauye na Mbunge wa Zenga Huessein Bashe kuwapeleka kwa Rais wakandarasi na wawekezaji wanaotaka kuwekeza kwenye Reli ya standard Gauge Hapa nchini.
Kauli ya Rais magufuli imekuja baada ya Wabunge hao kulalamika juu ya hatua ya serekali kujenga Reli hiyo kwa mkopo ambao unaipeleka nchi kuwa na deni kubwa la taifa kitu ambacho wanaona kulikua nahaja kwa serekali kutoa fursa hiyo kwa kampuni binafsi za ujenzi. wakichangia hoja wakati wa uwasilishaji wa mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa mwaka 2018/2019
Taarifa ya Rais magufuli imetolewa leo na Waziri wa fedha na mipango Dr. Philip Mapango baada ya jana kupokea simu ya Rais Magufuli kuwa wakati anahitimisha mjadala huo alipigiwa simu na Rais Magufuli
"Naomba ninong'one na bunge lako Tukufu, Mh Rais aliposikia huu mjadala alinipigia simu alinambia hivi, Waziri mwambia ndugu yako Mh. Nape na Mh. Bashe nawataka sana hao wawekezaji kwenye ujenzi wa standard Gauge Railway, wawalete hata kesho nipo tayari kuwapa Reli ya kutoka Kaliuwa -mpaka au Reli ya Isaka- Mwanza au Reli ya Mtwara-mchuchuma hadi Liganga'' alisema Waziri Mpango kwa niaba ya Rais