- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI ASEMA WATU WA KIMARA HAWATALIPWA FIDIA KAMWE
Dar es salaam: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John pombe Magufuli ameapa kutotoa fidia kwa wakazi wote wa Kimara walibomolewa nyumba zao kupisha ujenzi wa Barabara kwa kuwa Serekali ilishinda kesi dhidi ya wakazi hao iliyoamuliwa katika mahakama kuu ya Tanzania.
"Mbunge anasimama hapa anasema tuwalipe fidia, wakati anajua kuwa fidia haipo, Serikali ilishashtakiwa Mahakama Kuu na ikashinda, hivyo hakuna mahali pengine mnapoweza kushtaki." amesema Rais Magufuli
Kauli hiyo ya Rais Magufuli ameitoa leo Jumatano Desemba 19, 2018 baada ya kufanya uzinduzi wa Ujenzi wa barabara nane kutoka Kimara Stop Over mpaka mbezi
"Kwa wale wanaotaka kwenda kuangalia na najua Mheshimiwa Mnyika amesoma sheria waende wakaangalie kesi namba 39 ya mwaka 1997 iliyofunguliwa Mahakama Kuu Mshtakiwa alikuwa Mwanasheria Mkuu na Serikali"
"Ndugu zangu fidia hakuna, hata uwende wapi huwezi kusinda, kesi hii ilishaamuliwa na Mahakama Kuu
Lengo ni kutengeneza miundombinu tena tumejenga barabara hii hapa kwenye jimbo la wapinzani kwa kuwa maendeleo hayana vyama" alimalizia Rais Magufuli