- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI AMTENGUA NA KUMTEUA TENA MKURUGEZI WA DART
Dodoma: Rais John Pombe Magufuli jana Octoba 10 ameshangazi watu baada ya kutengua uteuzi wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Mabasi ya Mwendokasi (Dart), Ronald Lwakatale na kumteua Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) Mkoa wa Singida, Leonard Kapongo lakini dakika kama 10 hivi baadae akabatilisha uamuzi huo na kumrudisha kazini tena.
Hali hiyo imetokea Baada ya Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo alipowaambia waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu kutenguliwa kwa mkurugenzi huyo.
Alisema hata hivyo hivi karibuni kumekuwa na mdororo mkubwa na kwamba jambo hilo haliridhishi kabisa.
“Jambo hili katika ofisi yangu halitutiii amani kabisa. Kutokana na hilo Mheshimiwa Rais ambaye ni mwenye dhamana tawala za mikoa na Serikali za mitaa ameridhia kutenguliwa kwa mtendaji mkuu wa wakala huo Mhandisi Ronald Lwakatare na yeye atapangiwa kazi nyingine.” .
“Nafasi yake itachukuliwa na Mhandisi Leonard Kapongo ambaye ni Meneja wa Tanroad Mkoa wa Singida na uteuzi huo unaanza leo mara moja. Jukumu lake kubwa sasa atakwenda kuweka utaratibu mzuri wa kurudisha hali nzuri ya usafiri katika jiji la Dar es Salaam.”
Baada ya kumalizika kwa mkutano huo, waandishi waliondoka na walipofika getini walielezwa na walinzi kwamba wanaitwa tena na Waziri Jafo.
Mara baada ya kurejea, Jafo alizungumza tena na waandishi akisema kuna mabadiliko kuhusu taarifa hiyo kwamba mkurugenzi huyo aliyetumbuliwa ataendelea na shughuli zake kama kawaida ila anatakiwa kujitathimini.