Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 4:47 am

NEWS: RAIS MAGUFULI AKUBALI OMBI LA KUJIUZULU KWA KINANA

Dodoma: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli ameridhia ombi la kujiuzulu kwa aliyekuwa kaibu mkuu wa chama hicho Ndugu Abdulrahman Kinana ya kumuomba kujiuzuru nafasi hiyo aliyoiwasilisha jana May 27 ambapo Rais Magufuli ameisoma barua hiyo mbele ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) iliyokutana ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Mei 28, 2018.

Julai 2016, katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM ambao Rais mstaafu Jakaya Kikwete alimkabidhi uenyekiti wa CCM Rais Magufuli, ikiwa ni miezi minane tangu aingie madarakani, Kinana aliwasilisha barua ya kujiuzulu nafasi hiyo, lakini kiongozi huyo wa nchi aliikataa akimwomba amsaidie kwa sababu ya uzoefu wake.

Rais Magufuli, pia aliwataka manaibu katibu wakuu wawili na sekretarieti nzima ya chama hicho, kuendelea na kazi.

Watu wake wa karibu wanasema kuwa uamuzi wa Kinana kuomba kuondoka katika nafasi hiyo, unatokana pamoja na sababu kuwepo kwa mambo ambayo hashirikishwi.

Inaelezwa miongoni mwa mambo ambayo Kinana anaona hakushirikishwa kwa nafasi yake na amepata kusikika akisikitika kwa watu wake wa karibu, ni suala zima la uundwaji wa kamati kuchunguza mali za CCM.

Tayari ripoti ya kamati hiyo ilikabidhiwa kwa Rais Magufuli hivi karibuni na kimsingi huenda ikajadiliwa na wahusika kuchukuliwa hatua katika vikao hivyo vinavyoanza kuketi kesho.

Jambo jingine ni uteuzi wa wagombea ubunge katika majimbo ya Siha na Kinondoni, ambalo wana CCM wengi pia walilamika kuwa utaratibu wa chama hicho ulikiukwa.

Hata kabla ya Kinana hajaomba kujiuzulu, mjadala wa yeye kuondoka kwenye nafasi hiyo licha ya kudumu kwa muda mrefu na hata wakati fulani kutulia, ulirejea tena kwa kasi juzi na jana baada ya Rais Magufuli kuonekana akifanya vikao bila yeye kuwapo.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, ilieleza Rais Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na Mangula.

Pasipo kufafanua, taarifa hiyo ilieleza viongozi hao wamezungumzia masuala mbalimbali yanayohusu CCM na Serikali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akisoma barua ya Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana (kulia) ya kumuomba kujiuzuru nafasi hiyo mbele ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) iliyokutana ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Mei 28, 2018. Kushoto ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM (Visiwani) Dkt. Ali Mohamed Shein.

Kushoto ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM (Visiwani) Dkt. Ali Mohamed Shein.