- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI AGOMA KUPOKEA USHAURI WA MKAPA
JOHN Pombe Magufuli, mwenyekiti wa taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), “amegoma” kutekeleza ushauri wa rais mstaafu, Benjamin Mkapa,
Taarifa kutoka ndani ya chama hicho tawala zinasema, Mkapa alimtaka Rais Magufuli, kufanya mabadiliko ya uongozi wa juu wa chama chake kwa kuwapumzisha baadhi ya viongozi wandamizi na kuingiza damu mpya.
Miongoni mwa waliotakiwa kupumzishwa, ni makamu mwenyekiti wa chama hicho, Tanzania Bara, Philiph Mangula. Mwingine aliyetakiwa kupumzishwa, ni katibu mkuu wake, Abdulrahaman Kinana.
Mkapa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka 10, alimtaka Magufuli kumpimzisha Mangula, kwa maelezo kuwa tayari amezeeka na hivyo angeweza kukisaidia chama hicho kwa ushauri akiwa nje ya uongozi.
Kwa upande wa Kinana, mtoa taarifa anasema, rais huyo mstaafu wa awamu ya tatu, alimtaka Magufuli kumkabidhi wadhifa wa makamu mwenyekiti Bara.
“Mzee Mkapa alimtaka mwenyekiti wake wa taifa (Rais John Magufuli), kumpumzisha Magula kwenye nafasi ya makamu mwenyekiti Bara. Alisema, Magula ameshazeeka na hivyo hawezi kukisaidia chama hicho akiwa ndani ya uongozi,” anaeleza mtoa taarifa
Philiph Mangula
Anasema, “Mzee Mangula angeweza kusaidia sana chama kama angekuwa mshauri; anayetoa ushauri wake nje ya jukwaa la uongozi.
“Akamtaka pia kumbadilishia majukumu Kinana kwa kumtoa kwenye nafasi ya katibu mkuu na kumkabidhi nafasi ya makamu mwenyekiti kwa sababu zilezile za umri.”
Anasema, “lakini mwenyekiti amegoma. Amemrudisha Mzee Mangula kwenye nafasi yake. Sijui kwa nini amekataa ushauri huo.”
Anaongeza, “yawezekana anapeleka ujumbe kuwa anataka kuwa huru katika kuendesha chama na serikali. Kwa maneno mengine, pengine hataki kuingiliwa katika utendaji wake wa kazi.”
Yusuf Makamba
Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja wiki moja tokea aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba, kuhutubia mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma na kumsifu kiongozi huyo kuwa amekuwa anasimamia bila woga kile anachokiamini.
Makamba ambaye alikuwa katibu mkuu wa CCM kati ya mwaka 2006 hadi 2011, aliuambia mkutano huo mkuu kuwa aliwahi kutoa ushauri kwa mwenyekiti wake huyo juu ya uendeshaji wa chama, lakini aligoma kuutekeleza.
Alisema, “kuna siku nilikutumia meseji ukaniambia ushauri mbovu huutaki, hivyo ndivyo inavyotakiwa mimi sikukasirika. Kazi yetu sisi tuliowahi kuwa wajumbe wa Kamati Kuu (CC), ni kukushauri.”
Alisema, “kuna baadhi ya watu wamekuwa wakisema, sisi tuliowahi kuwa viongozi wa chama hiki, hatutaki kukushauri. Napenda kusema, hilo siyo kweli.”
Makamba ambaye ni hodari katika uzungumzaji wa kutumia vitabu vya dini aliamsha shangwe aliposema, “…mimi niliwahi kukushauri. Ukaniambia Mzee Makamba, ushauri wako nimeusikia, lakini sitaupokea kwa kuwa ni ushauri mbovu.”
Alisema, “tunakufahamu kuwa wewe una uwezo mkubwa wa kazi ya urais na ndiyo maana Kamati Kuu, ilipokutana ikakupendekeza. Unastahili kuwa mwenyekiti wa CCM kwa kuwa moja ya matatizo tunayoyapata ndani ya CCM ni watu kutosema ukweli, wanageuza matatizo, fitina ndiyo ukweli.”
Alisema, “nilipotoa ushauri wangu na haukupokelewa, mimi sikukasirika…kazi yetu ni kushauri…mtekelezaji ni wewe.”
Makamba alitoa kauli hiyo, wakati akitoa salamu kwa wajumbe wa mkutano mkuu. Alisifu msimamo wa mwenyekiti wake, kwa maelezo kuwa amekuwa akisimamia yale anayoaamini bila woga ikiwamo kukataa ushauri ambao anaona hauna tija.
chanzo mwanahalisi