Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 5:22 pm

NEWS: RAIS MAGUFULI AGAWA VITAMBULISHO 670,000 KWA WANYABIASHARA WADOGO

Dar es salaam: Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania John pombe Magufuli, ameamua kuzindua vitambulisho 670,000 kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo wadogo ili viwasaidie kuzitambulisha biashara zao popote walipo hapa nchini.

Rais Magufuli amegawa vitambulisho hivyo leo Jumatatu Desemba 10, alipokuwa katika mkutano wake na viongozi wa Mamlaka yaMapato (TRA) na wakuu wa mikoa ambapo amesema vitambulisho hivyo ni maalumu kwa wafanyabiashara ambao mtaji wao hauzidi Sh milioni nne.

“Nimefikia hatua ya kutoa vitambulisho hivyo mimi mwenyewe kwa sababu nimeona mamlaka husika inachelewesha na wafanyabiashara wadogo wanaendelea kusumbuliwa.

Rais Magufuli amesema vitambulisho hivyo viko 670,000 na kila mkuu wa mkoa atapewa vitambulisho 25, 000 ili wakavigawe kwa wafanyabiashara wa maeneo yao na fedha watakazopewa wakazilipe TRA.

“Vitambulisho hivi navitoa bure ila wafanyabishara watachangia 20,000 kila mmoja, kama kurudisha gharama yautengenezwaji wake ili fedha hizo zikatumike kutengenezea vitambulisho vinginena kianze kutumika mara tu anapokipata.

“Kama vitambulisho hivi navitoa mimi mwenyewe sijaona mtu wa kuwasumbua, na mfanyabiashara mwenye mtaji wa chini ya Sh 4,000, 000 na ana kitambulisho nasisitiza asisumbuliwe,” amesema