Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 7:30 pm

NEWS : RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE WA MAKATIBU

#BREAKING RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE

Rais Magufulileo October 26, 2017 amefanya uteuzi katika nafasi za Naibu Makatibu Wakuu, Makatibu Wakuu na Wakuu wa Mikoa huku akiteua Naibu Makatibu Wakuu wapya saba, wanne wamekuwa Makatibu Wakuu, kawahamisha wanne na Naibu mmoja na Mabalozi.

Rais amewateua aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Dr Aziz Mlima na aliyekuwa IGP, Ernest Mangu kuwa Mabalozi ambapo vituo chake kitatangazwa baadaye.

Aidha, Rais Magufuli ameteua Wakuu wapya wa Mikoa mitatu; Rukwa, Manyara na Geita baada ya waliokuwepo awali kustaafu ambapo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexandder Pastory Mnyeti, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara huku aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Joackim Wangabo akiteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.

Robert Gabriel ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita huku Mkoa wa Mara, ameteuliwa Naibu Waziri wa Fedha wa zamani, Adam Kigoma Malima kuwa Mkuu wa Mkoa huo.

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Christina Mndeme ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Gelasius Byakanwa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, kabla ya hapo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai.

Aidha, MaRC walioondolewa katika nafasi zao ni Jordan Rugimbana aliyekuwa Dodoma, Halima Dendego aliyekuwa Mtwara na Dr Charles Mlingwa aliyekuwa Mara huku MaRC waliostaafu ni Joel Bendera (Manyara), Zelote Stephen (Rukwa)
na Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga (Geita).