Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 11:53 am

NEWS: RAIS MAGUFULI AELEZEA SABABU YA KUTUMBUA WATU

Dar es Salaam: Rais John Pombe Magufuli amesema hapendi kusikia neno kutumbua lakini analazimika kufanya hivyo kulingana na baadhi ya wateule wake kutomuelewa anataka nini.

Kauli hiyo ameitoa leo Jumamosi Septemba 29, 2018 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa kumuapisha Naibu Waziri mpya wa Mambo ya Nje, Dk Damas Ndumbaro aliyemteua siku tatu zilizopita.

“Najaribu kuzungumza hili kwa uwazi ili watu wasije kufikiria mimi napenda sana kutumbua, tena siku hizi sipendi hata kulisikia hilo neno kutumbua,” amesema Rais Magufuli.

“Lakini nitafanyaje mtu unamteua pale na hakuna kinachotokea, wengine unaona wanahangaika ila yeye yupo tu,sasa nataka Dk Ndumbaro ukafanye kazi.”

Rais Magufuli alimteua Dk Ndumbaro kuchukua nafasi ya aliyekuwa naibu waziri wa wizara hiyo, Dk Suzan Kolimba ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Dk Ndumbaro ni mbunge wa Songea Mjini.