Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 3:53 am

NEWS: RAIS KENYATTA AWATAKA WALIOTAFUNA PESA ZA UMMA KUREJESHA

Nairobi: Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewataka wale wote wanaodaiwa kuiba fedha za umma zinazokadiriwa kuwa Dola Milioni 80 kutoka Shirika la huduma kwa vijana NYS, wabebe mizigo yao wenyewe na wasimlaumu yeyote.

Kenyatta amesema serikali yake itahakikisha kuwa fedha zilizoibiwa zinarejeshwa.

Tayari washukiwa 24 kati ya 54 wamefikishwa Mahakamani, na kukanusha madai dhidi yao.

Watuhumiwa 24 walioshtakiwa kuhusiana na kashfa hiyo ya ufujaji wa pesa katika Shirika la Vijana wa huduma kwa Taifa (NYS) watakaa rumande kwa wiki moja. Uamuzi huo ulichukuliwa na jaji, ambaye

aliamuru wazuiliwe hadi wiki ijayo ambapo uamuzi wa kuachiliwa kwa dahamana utatolewa.

Miongoni mwa walioshtakiwa siku ya Jumanne ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana na Jinsia Lilian Mbogo Omollo na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Richard Ndubai.

Lilian Mbogo Omollo pia alikua afisa mhasibu wakati malipo hayo ya ulaghai yalipotolewa

Walikamatwa na wengine wakajisalimisha kwa polisi Jumatatu wiki hii na kisha kufikishwa mahakamni Milimani, Nairobi siku ya Jumanne wiki hii.