Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 4:36 pm

NEWS: RAIS KENYATTA AKUTANA NA MBAYA WAKE ALIYE FUTA UCHAGUZI

Nairobi: Rais wa kenya Uhuru Kenyatta jana amekutana na Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga na kupeana mikono hii na kwa mara ya kwanza tangu Jaji Huyo kufuta matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8 mwaka huu.
Kenyatta mara nyingi ameonekana akimtumia lawama Jaji Maraga kutokana na uamuzi wake wa kubatilisha matokeo hayo yaliyompa ushindi ambayo Kenyatta anaona kama yalifanyika mapinduzi ya watu wanne dhidi ya wananch wa kenya.

Lakini baada ya kukutana wawili hao na kupeana mikono walikaa katika jukwaa moja wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa nakuwa kivutio kikubwa zaidi
Walipeana mikono huku kila mmoja wao akionyesha sura ya tabasamu. Tukio hilo liliwavutia wananchi wengi huku vyombo vya habari vikionekana kulipa uzito zaidi. Nao viongozi waliokuwa wameketi meza kuu waliwageukia wawili hao wakistaajabu kuona jinsi walivyopeana mikono.


Sherehe hizo za jana zilihudhuriwa pia na Naibu Jaji Mkuu, Philomena Mwilu. Pia, walikuwemo Makamu wa Rais William Ruto na spika wa bunge Justin Muturi.
Kambi ya Nasa inayoongozwa na Raila Odinga ambaye amesusia uchaguzi wa marudio hawakuhudhuria.

Kenya inakusudiwa kufanya marudio ya Uchaguzi oktoba 26 mwaka huu, huku upande wa upinzani Nasa ikipinga kufanyika kwa uchaguzi huu na kuitisha maandamano tarehe hiyo iliyopangwa kufanyika kwa uchaguzi huo.