- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS KAGAME AFUMUA UPYA BARAZA LA MAWAZIRI
Rais wa Rwanda Paul Kagame amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri huku stori kubwa ni kumfuta kazi Rafiki yake Jenerali James Kabarebe Katika Wadhifa wake kama waziri wa Ulinzi na kumteua Dkt Richard Sezibera kuwa waziri mpya wa mashauri ya nchi za nje.
Jenerali James Kabarebe aliyekuwa mtu wa karibu sana na Rais Kagame amepoteza wadhifa wake Rais Kagame amemteua kama mshauri wa rais katika masuala ya usalama.
Jenerali Kabarebe ambaye amepewa nafasi ya kuwa mshauri maalumu wa rais wa maswala ya ulinzi na jeshi alikuwa mshirika wa karibu sana na Rais Paul Kagame tangu vita vilivyong'oa utawala wa rais Juvenali Habyarimana miaka ya 1990.
Katika mabadiliko makubwa na ya kushtukiza aliyofanya Rais Kagame wizara 8 kati ya 23 zimepata mawaziri wapya zikiwemo wizara nyeti tatu, wizara ya ulinzi ambayo sasa inaongozwa na Meja jenerali Albert Murasira aliyechukua nafasi ya Jenerali James Kabarebe.