- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: PROF. MBARAWA AKASIRISWA NA WAKANDARASI WABABAISHAJI KWENYE MIRADI
Mtwara: Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa ameoneshwa kukerwa na wakandarasi wababaishaji wanao changia miradi mingi ya maji kuchelewa kukamilika au kujenga miradi yenye viwango duni na kuisababishia Serikali hasara na kuigombanisha na wananchi wake.
Mbarawa amekasirishwa baada ya kukosekana kwa mkandarasi katika eneo la kazi kwenye mradi wa Nanyamba-Mlanje, katika Wilaya ya Nanyamba mkoani Mtwara wakati alipofika kukagua mradi, kitendo ambacho hakukifurahia.
Profesa Mbarawa amesema alitegemea kumkuta mkandarasi huyo site ili aweze kuzisikia changamoto zinazomkabili na kuzipatia ufumbuzi ili mradi huo uweze kukamilika mara moja na kutoa huduma.
Akiongea na wakazi wa Mlanje, Profesa Mbarawa amesema ametoka kuidhinisha malipo ya Shilingi Milioni 93 kwa mkandarasi huyo wiki iliyopita lakini ameshangazwa na kutomkuta akifanya kazi, na kuwaambia wakandarasi wasiokaa site ni wababaishaji na hawafai.
“Wakandarasi wa namna hii ni wababaishaji hawatufai na siwataki kwa sababu wanaigombanisha Serikali na wananchi, wakikwamisha mipango ya Serikali na wananchi wakiendelea kukosa maji bila sababu za msingi. Sitaki wakandarasi wa aina hii na ndio maana tumewafukuza waliokuwa kwenye miradi ya Kigoma na Lindi kutokana na tabia za ubabaishaji’’, amesema Profesa Mbarawa.