Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 11:36 am

NEWS: PROF KABUDI AWATAKA WANASHERIA KUTUMIA FURSA VIZURI.

DODOMA: Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi amewataka wanasheria nchini kutumia fursa zilizopo ilikuleta mabadiliko chanya katika sekta ya sheria.


Ametoa kauli hiyowakati wa mkutano wa wizara ya katiba na sheria na wakuu wa taasisi , idara na vitengo vya sheria serikali uliofanyika leo mjini hapa.

‘’Mara nyingi tunapotenza mwelekeo kwa sababu hatutumii fursa zilizopo,’’amesema kabudi.

Kabudi amesema ili kufikia lengo ni lazima wanasheria katika taasisi , idara na vitengo vya sheria kufanya kazi kwa ushirikiano.

Aidha ameongeza kwa kuwataka watendaji hao kujenga mahusiano mazuri kati yao ili kuboresha ufanisi katika utendajiwa kazi ndani ya Taifa.

‘’Sisi ni kitu kimoja ni lazima sekta hii ipate taarifa kutoka kwa taasisi mbalimbalisheria ni kitu mtambuka,’’amesema .

Mbali na hayo amesema lego la mkutano huo ni kujenga nia ya kuthaminia kati yao, kujenga uongozi shirikisho, kujenga‘team work’, kujenga moyo wa ushirikiano.

Kabudi Ameongeza kuwa lengo nyingine ni kujenga mahusiano kati ya taasisi na idara, kujadili mwelekeo wa sheria.

‘’Ili mabadiliko yaje ndani ya sekta ya sheria ni lazima kutengeneza sekta bora ili kutatua changamoto zilizopo,’’ameongeza kwa kusema.

Hata hivyo amesema kuwepo kwa wanasheria nchini lengo la serikali kuwa na nguvu muhimu ya utendaji wa serikali.

‘’Ni lazima kuwa wabunifu ili mchango wetu uonekane katika utendaji,’’ameeleza Kabudi.