Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 2:26 pm

NEWS: PORI LA AKIBA LAWALIZA WANANCHI WA KIJIJI CHA KEIKEI.

KONDOA DOM: Wakazi wa kijiji cha Keikei kata ya keikei wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma wameilalamikia Wizara ya maliasili na utalii kuwapora eneo lao la malisho,maji na kilimo lililokuwa katika mbuga ya hifadhi ya Mkungunero.

Wamesema changamoto hiyo ilianza mara baada ya kubadilisha kutoka kwenye pori tengefu kuwa pori la kiba na kudai wakati wa ubadilishaji hawakushirikishwa.


Akizungumza kwenye ziara ya Katibu wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) kanda ya kati (singida na Dodoma) Dominic Bruno alipotembelea kijijini hapo moja ya wafugaji Yahaya Athumani amesema pori hilo lilikuwepo tangia enzi za utawala wa Mwalimu nyerere na kudai kuwa chanzo ni mabadilio ya pori hilo.

"Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa walikaa na wazee wetu wakakubaliana na kuweka bikoni namba sita lakini cha kushangaza saivi tunapigwa danadana ramani ya zamani ilikuwepo na inafahamika hii ramani mpya haina mwelekeo,’’amesema Athumani.

Akiwatoa hofu wananchi hao katibu wa Chama cha Wafugaji Tanzania(CCWT) kanda ya kati (Dodoma na Singida )Dominic Bruno alisema ilipofika 1996 pori tengefu la mkungunero lilipandishwa hadhi likawa pori la akiba kinacholeta utata ni kutokujua wakati wa kupandishwa ramani walitumia ramani ipi ile ya zaman au la, pia alisihi wananchi hao kuwa na Subira Serikali ipo na inaendelea kulifanyia kazi

Akinukuu maneno ya Waziri Kigwangalla Katibu huyo amesema ‘’Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla jana tarehe 7 februari, 2018 ametembelea Pori la Akiba Mkungunero katika Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma na kuwataka wananchi wanaozunguka pori hilo kusubiri uamuzi wa Serikali utakaoshirikisha Wizara yake, Wizara ya Ardhi na Tamisemi katika kujibu maombi yao ya kutaka kupewa sehemu ya ardhi katika pori hilo kwa ajili ya kuendesha shughuli za kibinadamu’’

"Nimefika hapa leo kujifunza juu ya mgogoro huu, nimejionea hali halisi lakini pia nina maelezo ya wataalamu ambayo yapo kwenye maandishi naomba niende nikayasome, niyatafakari ili niweze kushauriana na wenzangu na mwisho wa siku tuweze kuja na suluhu ya namna ya kuondokana na changamoto ambazo zimekuwepo’’.

"Niwaombe sana wakati Serikali inaendelea kutafuta suluhu ya mgogoro huu ni vema tukafuata sheria zilizopo, tuzingatie mipaka iliyowekwa ili tusiingie kwenye migogoro, lakini kwa sasa siwezi kwa namna yeyote ile kutamka neno la kujibu maombi ya mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji na wananchi yaliyotolewa hapa leo.

"Kama Serikali tutakaa, Wizara yangu, Wizara ya Ardhi na Tamisemi ili tujue kiini cha mgogoro huu tufanye uamuzi kuwa ni maeneo gani yaongezwe katika hifadhi kwa ajili ya wananchi au ni vitongoji vipi vifutwe, tutaleta majibu, na jambo hili tutalifanya kwa uadilifu mkubwa bila kumuonea mtu ili kumaliza mgogoro huu," ameendelea kunukuu Katibu huyo.

Pori la Akiba Mkungunero ambalo lina ukubwa wa Kilimita za Mraba 557.9 lina umuhimu mkubwa kiuchumi na kiikolojia kwa kuwa ni chanzo muhimu cha mto Tarangire ambao ni uhai wa hifadhi ya Taifa ya Tarangire na ikolojia nzima ya ziwa Manyara. Pori hilo pia ni sehemu ya mapito na mazalia ya wanyamapori pamoja na makazi ya wanyamapori adimu duniani.