Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 7:51 pm

NEWS: POLISI YATAJA SABABU YA KUMKAMATA MWENYEKITI WA CHADEMA MBEYA

Mbeya. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei ametoa sababu ya msingi ya kumkamata mwenyekiti wa Chadema katika jiji la Mbeya, Obadia Mwaipalu kuwa ni kutaka kumuonya yeye na viongozi wenzake dhidi ya maneno yenye viashiria vya uvunjifu wa amani na uchochezi wanayoyatoa kwenye majukwaa ya kampeni za uchaguzi mdogo wa marudio unaoendelea jijini hapa. Mwaipalu alikamatwa na polisi alfajiri ya kuamkia jana na kupelekwa kituo kikuu cha polisi kabla ya kupelekwa kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RC0) Mkoa wa Mbeya, Modestus kwa ajili ya mahojiano. Related image

Akizungumza jana Sept. 4 , Kamanda Matei alisema licha ya kampeni hizo kuendelea kwa amani na utulivu, zipo taarifa za kiintelijensia za kuwapo kwa matumizi mabaya ya maneno yenye mrengo wa kichochezi yanayotamkwa na viongozi hao kwenye majukwaa ya kampeni. “Tumemuita huyo bwana Mwaipalu kumsihi yeye na viongozi wake watumie maneno ya staha, maana wamekuwa na maneno yenye mrengo wa kichochezi lakini tulipomhoji basi tumemuachia.

Image result for kamanda Ulrich Matei

Kweli tunazo taarifa za kiintelijensia na wengine tuna ushahidi wa kutosha kuhusiana na maneno wanayoyatoa kwenye majukwaa yao ya kampeni na tumewaita tumewafungulia kesi mahakamani na majalada ya uchunguzi dhidi yao tunaendelea nayo,” alisema kamanda huyo na kuongeza: “Kumleta mtu kituoni ni utaratibu wetu wa kawaida na huwa tunafanya hivyo pale tunapopata taarifa za kiintelijensia. Na yeye tulimuita ili kumkumbusha kwamba tunahitaji watumie lugha zenye kufuata misingi ya amani na si za uchochezi.” Alisema katika kipindi hiki cha kampeni, polisi wataendelea kufuatilia kwa karibu mikutano yote inayoendelea. “Tunawakumbusha wapiga kampeni kuepuka kutoa maneno yanayochochea uvunjifu wa amani, atakayekiuka hata akiwa ni wa CCM tutamuita tu na tayari tulishawahi kumuita kiongozi mmoja wa CCM,” alisema Kamanda Matei.