Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 2:40 am

NEWS: POLISI YAMTAKA ZITTO KUDHIBITISHA MAUWAJI WATU 100 KIGOMA

Kigoma: Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma limemtaka mbunge wa Kigoma Mjini kupitia ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe kudhibitisha mbele ya Jeshi hilo kwa kuwasilisha vielelezo vya madai yake kuwa yametokea mauaji eneo la Nguruka wilayani Uvinza mkoani humo na watu 100 walifariki Dunia.

Kama utakumbuka juzi siku ya Jumapili Oktoba 28,2018, Mbunge huyo alizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na kudai kuwa takribani siku 10 zilizopita yalitokea mauaji hayo na taarifa alizonazo ni kuwa watu zaidi ya 100, wakiwamo polisi walikufa.

Lakini kwaupande wa Jeshi hilo Jana Jumanne, Oktoba 30, 2018, Kamanda wa polisi mkoani Kigoma, Martin Ottieno amezungumza na waandishi wa habari na kukanusha tuhuma alizotoa Zitto na kusema hazina ukweli wowote.

Amesema hakuna watu 100 waliouawa na kusisitiza kuwa ni upotoshaji unaofanywa na wanasiasa.

“Hakuna watu mia moja waliouawa. Tunamtaka Zitto aonyeshe vielelezo vya hayo anayosema au aje atuonyeshe makaburi ya watu hao anaosema wameuawa Kigoma, ”amesema Ottieno.

Kamanda huyo amewataka wanasiasa kuchukua tahadhali kwa taarifa wanazopewa na watu mbalimbali kabla ya kuzisambaza ili kuepuka kupotosha jamii