Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:26 pm

NEWS: POLISI UFARANSA KULIPWA BONASI YA EURO 300

Serikali nchini Ufaransa jumanne ya Jana imependekeza kuwalipa bonasi ya euro 300 maafisa wa polisi ambao wamekuwa wakizuia maandamano ya vurugu nchini humo.

Ahadi hiyo ya serikali imetolewa siku moja baada ya vyama viwili vya wafanyakazi ndani ya kikosi cha polisi kutishia kuzorotesha kazi na kulalamika juu ya uhaba wa polisi wa kutosha na masuala mengine yanayohusu bajeti ya polisi.

Haijulikani bado kama bonasi hiyo a euro 300 itapunguza hasira miongoni mwa maafisa wa polisi wa ngazi za juu.

Baada ya masaa matatu, mazungumzo yaliahirishwa jana kati ya wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi vya kikosi cha polisi na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani. Mazungumzo hayo yanatarajiwa kuendelea tena leo.