- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: POLISI MARA YAZIHOFIA CHECHE ZA ZITTO NA HECHE
Tarime: Polisi mkoani Mara wameusambaratisha mkutano mkubwa wa kumnadi mgombea udiwani kata ya Turwa, (Chadema) ambao ulitakiwa kuhutubiwa na Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo) Ziito kabwe, Mbunge wa Tarime vijijini John Hechi na Mbunge viti maalum chadema Upendo Peneza
Mkutano huo umeshindwa kufanyika baada ya polisi kuwatawanya kwa mabomua ya machozi wafuasi wa vyama vya upinzani waliohudhuria mkutano huo.
Nae Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na wananchi wengine zaidi ya 10 wamekamatwa na polisi akiwamo mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Sita Tuma ambaye pia amekamatwa.
Kupitia ukurasa wa twitter wa Zitto amesema kuwa kunaamri kutoka juu ikimzua mbunge huyo asihutubie wananchi hao “ nisisikie huyo anaongea popote. Ana sumu mbaya sana na hana adabu”. Amri hiyo kama nilivyoambiwa ‘verbatim’. Mimi: kwanini mnaogopa maneno yangu? Acheni woga, tujadiliane tu mustakabali wa nchi. Anyways, Nipo salama. Nahangaika kuwatoa ndani mbunge Esther na Mwandishi Tuma"aliandika Zitto kabwe
Hata hivyo kamanda wa polisi mkoa wa Mara, Henry Mwaibambe hakupatikana kuzungumzia kamatakamata hiyo wala simu yake ya mkononi haikupokewa.
Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alitarajiwa kuhutubia mkutano huo.
Akizungumzia tukio hilo, katibu wa Chadema mkoa wa Mara, Chacha Heche amedai kwamba chama chake kimezuiwa kufanya mkutano wa kampeni kuanzia leo Agosti 8, 2018 hadi Agosti 11.
Hata hivyo Heche amesema chama hicho hakikupewa barua rasmi ya kuzuiwa kufanya mkutano huu wa kampeni.
“Walikuja asubuhi kwenye ofisi za chama wakitaka tusifanye mkutano lakini hakukuwa na sababu ya msingi ya sisi kutofanya mkutano,” amesema.
Hata hivyo Zitto amesema wataendeleza kampeni hizo kwa kushiriki mikutano ya kampeni ya NCCR-Mageuzi.
Kadhalika Zitto amesema polisi wamemzuia kumuona Esther kituo cha polisi anaposhikiliwa.