- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: POLISI KENYA WATAWANYA MKUTANO WA UPINZANI
Nairobi: Polisi nchini kenya wametumia mabomu ya kutoa machozi kutawanya watu waliokusanyika katika mkutano wa Muungano wa upinzani National Super Alliance(NASA),Muungano wa NASA umesema hautambui ushindi wa Bw Uhuru Kenyatta uchaguzi wa marudio wa 26 Oktoba mwaka huu, Mkutano wa NASA ulikuwa umepanga kufanya karibu sambamba na uwanja wa Jacarada, Nairobi.
Muungano huo unaoongozwa na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga ulisusia uchaguzi huo wa marudio ukisema haungekuwa huru na wa haki.
Polisi, ambao walikuwa wametangaza hakutakuwa na mkutano mwingine Nairobi kando na sherehe ya kuapishwa kwa Kenyatta, wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa upinzani waliokuwa wanakusanyika nje ya uwanja huo.