- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: POLEPOLE ASEMA VIONGOZI MIZIGO HAWATARUDI UCHAGUZI 2020
Zanzibar: Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole amewatahadharisha Viongozi wanaoshika nafasi za uwongozi kuwa hawakupewa nafasi hizo kwa ajili ya kula bata.
Pia Polepole amesema licha ya ushindi mkubwa wanaoendelea kuupata kwenye chaguzi mbalimbali, lakini hawatakua tayari kuwarudisha viongozi mizigo kwa wananchi katika uchaguzi mkuu mwaka 2020.
"Chama chetu hakikuwapa nafasi ya uongozo kama zawadi ili mwende mkale bata, tumewapa nafasi ya kuwatetea wananchi wenu na kutetea ilani ya chama chetu" alisema.
Polepole aliyasema hayo leo Jumanne Novemba 6, 2018 wakati akizungumza na wajumbe wa kamati za siasa mkoa na wilaya ya Kusini Unguja visiwani Zanzibar katika ukumbi wa mkutano wa TC Dunga.
Alisema wabunge na madiwani pamoja na wawakilishi wa CCM wanapaswa kujitathmini wakifahamu wana jukumu kubwa la kuwaletea maendeleo wananchi.
Pamoja na hayo, Polepole aliwataka watendaji wa Serikali wakiwamo wakurugenzi wa manispaa na viongozi wengine wa wilaya na mikoa kuhudhuria vikao vyote vya chama kueleza utekelezaji wa ilani ya chama katika majukumu yao.