- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: POLEPOLE AJINGAMBA KUISIMAMIA SERIKALI
Dar es salaam: Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Humphrey Polepole amekutana na viongozi wa wafanyabiashara wadogo wadogo wa soko la Kariakoo, Wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es salaam na kufanyanao Mazungumzo yenye lengo la kusikiliza kero zao, changamoto zinazowakabili na mashauriano ya fursa mbalimbali ikitafsiri muendelezo wa Chama kushughulika na shida za watu kwa vitendo.
Akizungumza na viongozi hao wa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga Jana Agosti 2 2018 Ndg. Polepole amesema CCM ipo tayari kushirikiana, kushauriana na kusaidia makundi mbali mbali ya kijamii katika kuhakikisha ustawi wa makundi hayo na msimamo wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) upo dhabiti katika kuhakikisha changamoto za wananchi zinapatiwa majibu.
"Ndg. Magufuli anawapenda sana wafanyabiashara, anapenda haki yenu ipatikane na haki ya Serikali pia ipatikane aidha kwa kulipa kodi ama tozo kwa mujibu wa sharia ili Serikali iendelee kuwa na uwezo wa kuhudumia wananchi" alisema Polepole
Kikao hiki cha kazi kati ya wafanyabiashara wadogo wadogo wa soko la kariakoo na CCM kitakuwa na muendelezo hivi karibu ambapo Chama kimesisitiza kuwakutanisha wafanyabiashara hao na wadau na mamlaka zote za Serikali zinazohusika na biashara ili kufanikisha utatuzi wa changamoto zao kwa kasi na uhakika.