- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: POLEPOLE AJIGAMBA CCM KUSHINDA UCHAGUZI WA MONDULI NA UKONGA
Dar es Salaam: Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama tawala CCM,Bw. Humphrey Polepole amesema chama cha mapinduzi kitashinda uchaguzi mdogo katika majimbo ya Ukonga na Monduli unaotarajia kufanyika Kesho kutwa Septemba 16, 2018
Akiongea na waandishi wa habari leo Septemba 14, 2018 Polepole amesema CCM imejitahidi kufanya kampeni za kistaarabu na wananchi wamejitokeza kwa wingi kuwasikiliza. "Tathmini ya awali inaonyesha kwamba mikutano yetu ya hadhara ilikuwa mikubwa mara tatu kuliko ile waliyofanya wenzetu," amesema. Polepole amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi na kukichagua chama tawala li kiwaletee maendeleo kwenye maeneo yao.
"Wachague wagombea wa CCM ili wakawe kiungo na Serikali katika kutatua kero zao. Ukichagua mgombea wa CCM, atashirikiana na viongozi wa Serikali kuleta maendeleo," amesema. Polepole amesema chama chake kinatoa elimu juu ya sheria za uchaguzi. Pia, amesema wanatoa elimu juu ya kanuni za uchaguzi za CCM. Amesema katika awamu hii, CCM imejipanga kufanya siasa safi za kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo. Amesema chama chake kimejipanga kutatua kero mbalimbali.