Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 11:41 am

NEWS: POLEPOLE AELEZEA SABABU ZA KUKWAMA KWA KATIBA MPYA

Dar es salaam: Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha CCM, Hamphrey Polepole amesema mchakato wa Katiba ulikwama kwa sababu hakukuwa na uelewa wa pamoja nini wananchi wanataka jambo ambalo, tayari limeshaeleweka ndani ya chama hicho.

Polepole amesema hayo leo Alhamisi katika kipindi cha Maisha Mseto kinachorushwa na redio Times FM, kuwa yeye ni muumini wa maoni ya wananchi kwenye mchakato wa Katiba mpya.

Amesema wakati ya mchakato wa Katiba mpya alikuwa miongoni mwa wajumbe waliokusanya maoni ya wananchi ataendelea kuunga mkono maoni yao.

“Nilikusanya maoni ya wananchi nchi nzima ya Tanzania na ninajua nini Watanzania wanasema kwa hiyo, mimi ni muumini wa maoni ya wananchi,” amesema.

Amesema mchakato huo ulikwama kwa sababu hakukuwepo na uelewa wa nini Watanzania wanataka.

Hata hivyo alidai kuwa mabadiliko makubwa yanayofanywa ndani ya chama hicho yanaakisi kushughulikia kero za wananchi.

“Siasa safi ni kushughulika na kero za wananchi wetu, chama kimejitathmini na kujisahihisha kwa sababu tumepata usahidi kwamba kuna mahali tulikosea kwa hiyo, tunao utaratibu wa kujikosoa,” amesema.