Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 3:31 am

NEWS: PAPA APIGA MARUFUKU UUZWAJI WA SIGARA MJI WA VATICAN

Italy: Papa Francis amepiga marufuku ya uuzaji wa sigara ndani ya mji wa Vatican ,amri hiyo itaanza kutekelezwa mwaka 2018

Greg Burke ambaye nimsemaji wa Vatican alisema kuwa mji huo mtakatifu hauwezi kukubaliana na kitendo ambacho kinahatarisha maisha ya binaadamu.

Zaidi ya wafanyikazi 5000 wa mji huo na wale waliostaafu wanaruhusiwa kununua sigara zilizopunguzwa bei.

Mauzo ya sigara hizo yanakadiriwa kuiletea Vatican mamilioni ya Euro kila mwaka.

Lakini bwana Burke amesema kuwa hakuna faida ambayo ni halali iwapo sigara zinaathiri afya za wanaadamu.

Burke alinukuu takwimu za shirika la afya duniani WHO ambazo zinalaumu uvutaji sigara kwa kusababisha vifo vya takriban watu miioni 7 duniani kila mwaka.

''Nadhani watu wengi wanapenda sigara kwa sababu ya ufadhili wanaopata'' ,alisema.

''Ni kitu ambacho ni lazima kufutilia mbali licha ya kuleta mapato Vatican, muhimu ni kufanya kile kilicho sawa''.