- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: OFISI YA TAKWIMU YANANG'ARA YAANZISHA MFUMO WA KIELEKRONIKI UTAKAOSAIDI KUKUSANYA TAAARIFA KWA URAHISI.
SASAJILA DOM: Ofisi Ya Taifa Ya Takwimu Kwakushirikiana Na Wizara Ya Ardhi,Wizara YaMaliasili Na Utalii,Tamisemi Imeanzisha Zoezi La Ukusanyaji Wa Taarifa Mbalimbali Kwakutumia Mfumo Wa Kisasa Wa Kielektroniki ambapo Mfumo huo Utasaidia Ukusanyaji Wa Taarifa Kwa urahisi na Kuokoa Fedha Tofauti Na Ilivyokuwa Awali.
Akizungumza na Waandishi Wa Habari Kuhusu Jinsi Mfumo huo Unavyofanya Kazi Katika Kijiji Cha Sasajila Kilichopo Wilaya Ya Chamwino Mjini Hapa Mrasimu Ramani Mwandamizi Na Msimamizi Wa Mfumo Wa Ukusanyaji Na Usambazaji Wa Taarifa Za Kijografia Benedict Mgami amesema Mfumo Huo Utasaidia Kupata Ramani Zitakazo Saidia Serikali Katika Shughuli Mbalimbali Za Maendeleo
Aidha Bw Benedict Ameongeza Kuwa Zoezi Hilo La Ukusanyaji Wa Taarifa Kwa Mfumo Wa Kidijitali Utasaidia Kuboresha Ukusanyaji Wa Takwimu Katika Kutenga Maeneo Pamoja Na Kuokoa Garama Za Fedha Na Muda Tofauti Na Zilizokuwa Zikitumika Awali Na Mfumo Huo Utasaidia Ukusanyaji Wa Taarifa Zitakazotumika Kipindi Cha Sensa Ya Watu Na Makazi Ya Mwaka 2020
Kwa upande Wake Mwenyekiti Wa Kijiji Cha Sasajila Bw, Mussa Samwel Mtukwa Amesema Kumekuwepo Na Changamoto Kubwa Ya Mipaka Kati Ya Vijiji Vitatu Ambavyo Ni Manzase, Sasajila Na Fufu Kutokana Na Kuongezeka Kwa Watu Nakuingiliana Kwa Mipaka Kiasi Cha Baadhi Ya Wananchi Kuvuka Na Kufanya Maendeleo Kwenye Vijiji Vingine Uku Akitoa Wito Kwa Serikali Na Vyombo Vya Habari Kushughurikia Swala Hilo
Akijibu Kuhusu Changamoto Hiyo Bw, Benedict Amesema Tatizo Hilo La Migogoro Ya Ardhi Lipo Maeneo Mengi Ya Nchi Lakini Wao Kupitia Zoezi hili Wanatunza Kumbumbuku Kuhusu Changamoto Wanazozikuta Katika Jamii Husika Ili Kuweza Kutatuliwa