- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ODINGA APANGA KUITISHA MAANDAMANO SIKU YA UCHAGUZI
Dar es salaam: Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya(NASA) Raila Odinga ameitisha maandamano ya nchi nzima tarehe 26 mwaka huu, kimsingi siku hiyo ndio siku ambayo Uchaguzi mpya wa urais umepangwa kufanyika na Tume ya Uchaguzi nchini humo.
Odinga amekazania msimamo wake kuwa Uchaguzi hauwezi kufanyika bila mabadiliko ndani ya Tume ya Uchaguzi na kama utakumbuka Kiongozi huyo wa upinzani alijitoa kwenye kinyang'anyiro cha Uchaguzi.
Mwenyekiti wa Tume hiyo ya Uchaguzi Wafula Chebukati tayari amesema kuwa anatilia shaka, iwapo uchaguzi huo utakuwa huru na haki iwapo viongozi wa kisiasa nchini humo hawatazungumza na kutatua mzozo wa kisiasa unaoendelea.
Wakati huo huo Rais Uhuru Kenyatta ameitisha maombi kabla ya marudio ya Uchaguzi, licha ya kusema baadaye kuwa hana cha kuzungumza.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa nchi itafanya maombi mwisho wa wiki hii kabla ya marudio ya uchaguzi mkuu wa wiki ijayo.
Taarifa ya Rais Kenyatta ilikuja baada ya afisa wa cheo ya juu kwenye Tume ya Uchaguzi Roselyne Akombe, kukimbia nchi akisema kuwa amekuwa akipokea vitisho vya kuuawa.
Rais Kenyatta alisema kuwa wakenya watatumia wikendi kwa maombi na maridhiano kabla ya marudio ya uchaguzi wa urais ambao umepangwa kufanyika tarehe 26 mwezi Oktoba.