- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: OBAMA AMEZAA KWA NJIA YA KUPANDIKIZA MBEGU
U.S: Aliyekuwa Rais wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle Obama kumbe walifanya jitihada za kupata watoto wao kwa njia ya kupandikiza uzazi inayofahamika kwa jina la IVF (In Vitro Fertilization )
Taarifa hiyo imefichuliwa na mkewe Michelle Obama kupitia kituo cha Runinga cha ABC good Morning wakati akitoa kumbukumbu ya matatizo aliyopitia katika ndoa yake na ujauzito wa watoto wake wawili.
Kupitia Katika kitabu chake cha , Becoming, Bi Obama amefichua kwamba alitokwa na ujauzito na akalazimika kutumia mbinu ya IVF ambapo mayai ya wapendanao huchanganywa nje na baadaye kuwekwa katika kizazi cha mwanamke kupitia sindano.
Bi Obama aliambia kituo cha ABC Good morning America kwamba alihisi 'amepotea na mpweke' baada ya kupoteza uja uzito miaka 20 iliopita.
Bi Obama , wakili wa zamani na msimamizi wa hospitali aliambia ABC kwamba baada ya kupoteza uja uzito, nilihisi kwamba nimefeli kwasababu sikujua takwimu za kumwagika kwa uja uzito.
''Tunajitenga tukiwa na uchungu'', alisema akiongezea kuwa ''ni muhimu kuzungumza na akina mama wachanga kuhusu ukweli kwamba uja uzito unaweza kukutoka''.
Bi Obama alifichua kwamba ndoa yao ilikumbwa na misukosuko mara nyengine , hususan baada ya mumewe kujiunga na bunge la jimbo hilo , na hivyobasi kumwacha nyumbani ambapo alilazimika kutumia sindano za IVF mwenyewe.
''Ushauri katika ndoa yetu kwetu sisi ulikuwa mojawapo ya njia ambapo tulijua kushughulikia tofauti zetu'', aliambia ABC.
''Najua wanandoa wengi wachanga ambao wanakabiliwa na changamoto na nadhani kuna makosa wanayofanya, Na nataka wajue kwamba bi Michelle na Barrack Obama ambao wamekuwa na ndoa nzuri na ambao wanapendana sana, pia huketi chini na kuimarisha ndoa yao. na tunapata usaidizi wa ndoa yetu tunapohitaji''.