- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NYAMAYAHASI:''KWA SASA 60% YA MAENEO HAYAJAWEKEWA MIPANGO YA MATUMIZI BORA YA ARDHI''.
DODOMA: Imeelezwa kuwa kwa sasa asilimia 60 ya maeneo hapa nchini hayajawekewa mipango ya matumizi bora ya ardhi.
Hayo yamesema na mwenyekiti wa jukwaa la wakulima wanawake Chamwino (JUWACHA) Janeth Nyamayahasi wakati wa kuwasilisha mapendekezo yao kwa kamati ya bunge ya kilimo,mifugo na maji leo mjini hapa.
Nyamayahasi amesema kumekuwa na upungufu wa vyanzo vya maji vinavyotumika kwa wakulima na wafugaji ,nakuiomba kamati hiyo kuishauri serikali kutambua na kutafuta vyanzo vipya vya maji na kuvitunza.
‘’Kuweka fedha zakutosha katika umwagiliaji na kuweka mazingira mazuri ya PPP ili kutumika na kuweza kushawishi uwekezaji katika miundombinu ya maji pamoja na usambazaji ,’’amesemaNyamayahasi.
Aidha aliiomba kamati kuishauri serikali kutoa maelekezo kwa wasambazaji wa pembejeo kufunga mbolea katika vipimo mbalimbali na si kilo 50.
‘’Hii itamsaidia mkulima asiye na uwezo wa kununua mfuko wa mbolea aweze kununua kwa kilo bila kuharibu ubora wake ni wajibu wa serikali kutatua tatizo hilo, Kuhimiza na kusimamia upatikanaji wa pembejeo kwa wakati,’’amesema.
Ameongeza kuwa tunapendekeza kamati kuishauri serikali kuanzisha bodi ya mazao mchanganyiko .
‘’Hivyo basi ili kuthibiti uporomokaji wa beina kuunganisha na masoko tunadhani kuanzishwa kwa bodi hii kutasaidia kama ilivyo kwenye korosho,pamba na tumbaku,’’ameongeza Nyamayahasi.
Hata hivyo ameiomba kamati hiyo kuishauri serikalikufuatia mchakato wa maandalizi ya bajeti kufuatwa na kuhakikisha vipaumbele vya wakulima na wafugaji pamoja na vile vya taifa vinatokea katika bajeti.
‘’Migogoro baina ya wafugaji na wakulima inasababishwa na kupungua kwa maeneo ya ufugaji,na kilimo cha kuhamahamana wawezeshaji kupewa maeneo makubwa ambayo hawayaendelezi,’’amesema Nyamayahasi.
Naye mbunge wa Hanang mkoani Manyara Mary Nagu amewataka wakulima hao kuwekeza katika kilimo cha umwagiliajiili hali wanasubiria serikali kutenga bajeti ambayo itawasaidia kujikwamua na kukuzasekta ya kilimo katika taifa letu
Kwa mujibu wa Takwimu za jukwaa hilo zinaonesha asilimia 65 wa watanzania kuajiriwa na sekta ya kilimo, mifungo na uvuvi, asilimia 29 kuchangia pato la taifa,asilimia 24 mauzo ya nje ,zaidi ya bidhaa asilimia 65 zinatoka kwenye viwanda na asilimia 40 upungufu wa maafisa ugani nchini.