Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 7:34 am

NEWS: NYALANDU ATISHIWA KUUWAWA KAMA TUNDU LISSU

Dar es salaam: Aliyekuwa Mbunge wa singida kaskazini na Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu amesema kuwa anapokea vitisho vingi tangu alipo kihama chama tawala cha CCM October 30, mwaka hu "Receiving unprecedented number of threats since leaving the ruling party CCM''.

Nyalandu ameseme kuwa wapo watu wengi wanaotumia nguvu kubwa kutaka kumnyamzisha, na ameomba watu kumuombea katika kipindi hichi kigumu anachopitia " It's incredible that there is so much panic from the elites, who are utilising all means possible to silence me. Please pray for me and my family during these trying times we face. alisema Nyalandu

Nyalandu alijiuzulu katika nyazifa zake zote kwenye chama cha CCM October 30, mwaka huu, nyazifa alizojiuzulu ni Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama.

Nyalandu alitaja sababu zilizomuondoa katika chama hicho kikongwe barani Afrika ambapo ni pamoja na kutoridhishwa kwake na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa HAKI za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA.

Hivi karibuni Waziri wa maliasili na utalii Hamisi kigagwala alitangaza kumfungulia mashitaka Nyalandu kutokana na kutumia madaraka yake vibaya wakati akiwa waziri wa maliasili na utalii, tuhuma ambazo alizikanusha kupitia mtandao wake wa Instagram "WAZIRI Kigwangalla ni shahidi wa UONGO anayedhani UONGOZI ni majigambo na ni haki kwake kutoa kauli za kejeli, uzushi, na zisizo za kweli. Kwa kumsaidia tu naomba alisikilize NENO hili lililoandikwa katika vitabu: "Mwenye kutawala akisikiliza UONGO, basi WATUMISHI wake WOTE watakuwa WAOVU." Mithali 29: 12." aliandika nyalandu