- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NYALANDU AFUFUA MAKABURI, ATAKA MCHAKATO WA KATIBA MPYA
Dar es salaam: Aliyekuwa waziri wa maliasili na Utalii na Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu amesema kuwa anania ya kupeleka muswada wa sheria Bungeni kutaka kuanzishwa kwa mchakato wa katiba mpya.
"NAKUSUDIA kuwasilisha kwa SPIKA wa BUNGE, Mh. Job Ndugai, Mb., AZMA yangu ya kuleta MUSWADA binafsi wa SHERIA katika KIKAO kijacho cha BUNGE itakayoweka SHARTI la kurejea UPYA mjadala wa KATIBA MPYA ya Tanzania'' alisema Nyalandu
Akizungumza jana kwenye mahafali ya Kidato cha IV, katika sekondari ya MWANAMWEMA Sekondari. Kijiji cha MGORI, SingidaKaskazini jana Nyalandu amesema kuwa atawasilisha muswada huo kwa kuzingatia Rasimu ya katiba ya Mzee warioba ''kwa KUZINGATIA RASIMU ya KATIBA kama ilivyowasilishwa na TUME ya JAJI WARIOBA"
Nyalandu ndio Mbunge pekee wa Chama tawala CCM kwenda Nairobi kumjulia hali mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu aliyeshambuliwa na Risasi Tarehe 7 septemba mwaka huu nyumbani kwake Mjini Dodoma