Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:36 pm

NEWS: NISSAN YASHINDWA KUMPATA MWENYEKITI MPYA

Bodi ya Wakurugenzi ya Nissan imeshindwa Jumatatu ya leo kuteua mrithi wa mwenyekiti wa wa zamani wa kampuni hiyo ya magari Carlos Ghosn aliyefutwa kazi kufuatia kukamatwa kwake tarehe 19 Novemba mjini Tokyo kwa kushtumiwa kupata mapato yasiyo halali.

"Bodi ya wakurugenzi imeamua kuendelea na mazungumzo" ya kamati ya wajumbe watatu wanaohusika na kupendekeza jina "na kuhakikisha jitihada zake kwa kuwajulisha kikamilifu washirika wake wa muungano wa kampuni, Renault na Mitsubishi Motors," Nissan imesema katika taarifa.

"Hatuna muda maalum wa mwisho katika fikra zetu. Hata kama uamuzi utakuwa haujachukuliwa mwishoni mwa mwezi Machi, nadhani itakuwa si tatizo." Amesema mkuu wa bodi ya uongozi Hiroto Saikawa, wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu ya kundi hilo huko Yokohama (kitongoji cha Tokyo).

Nissan pia imetangaza uundwaji wa "kamati maalum ya kuboresha utawala wa kapuni hizo", ambao kesi yake inagubikwa na mapungufu. Kamati hii, ambayo itakuwa na "kibarua kigumu" kulingana na Bw Saikawa, itaundwa na wakurugenzi watatu huru na wataalam wa kujitegemea.