- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : NIGERIA YAWATIA MBARONI WAUAJI WA KIKABILA
Serikali ya Nigeria yawatia mbaroni wahusika wa mauaji ya kikabila
Viongozi wa Nigeria wametangaza habari ya kutiwa mbaroni wahusika wa shambulizi la kikabila lililosababisha mauaji ya watu 50, mashariki mwa nchi hiyo.
Taarifa iliyotolewa na serikali ya Nigeria imesema kuwa, jeshi la polisi nchini humo limewatia nguvuni watu wanane ambao wamehusishwa na mauaji hayo yaliyowahusisha watu wa kabila la Fulani na wakulima katika eneo la Tif jimbo la Benue, mashariki mwa Nigeria. Katika shambulizi hilo lililotokea siku ya Jumanne iliyopita, watu 50 waliuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya wafugaji wa kabila hilo kuwashambulia wakulima.
Samuel Ortom, meya wa jimbo la Benue sambamba na kuthibitisha shambulizi hilo na kuikosoa serikali ya Nigeria kwa kutowalinda wakulima wa eneo la Tif, amesema, kabla ya kujiri shambulizi hilo aliwakumbusha viongozi wa ngazi ya juu serikalini juu ya uwepo wa vitisho vya wafugaji wa kabila la Fulani dhidi ya wakazi wa eneo hilo. Zaidi ya watu 300 wameuawa ndani ya kipindi cha miaka miwili iliyopita katika mapigano ya kikabila kati ya wafugaji wa kabila la Fulani na wakulima katika jimbo la Benue. Ukame, upungufu wa chakula, ongezeko la tofauti za kidini na kimadhehebu, ubaguzi wa serikali na kushindwa serikali kuu ya Abuja kudhibiti hali ya mambo, ni mambo yanayochangia kuongezeka vita vya kikabila ndani ya taifa hilo la magharibi mwa Afrika.