- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NEXT GENERATION MICROFINANCE YASHUSHA NEEMA YA FIMBO 30 KWA WATU WASIOONA.
DODOMA: Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu( kazi,vijana na ajira) Antony Mavunde amelitaka shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu(SHIVYAWATA) mkoani Dodoma kugawa fimbo kwa watu wasioona pasipo upendeleo ili kutenda Haki na kuleta usawa kwa wote.
Mavunde ameyasema hayo Leo mjini Dodoma alipokuwa akikabidhi fimbo 30 kwa chama cha watu wasioona (TLB) cha Mkoa wa Dodoma huku akiwataka kutovunja moyo makampuni au taasisi zinazojitolea kutoa msaada kwa watu wenye uhitaji na kudai kuwa wajibu sasa wakufanyakazi pasipo kumwangalia mtu wala upendeleo kwa mtu yeyote ili kila moja aweze kunufaika.
Awali akizungumza Meneja mkuu wa next generation microfinance Sospeter Kansapa amesema wao kama next generation wanaamini vifaa hivyo vitasaidia katika shughuli zao za kimaendeleo na ni moja ya chachu katika kuleta maendeleo ya Taifa letu.
Aidha amesema ili kuunga mkono jitihada za rais John Magufuli ni jukumu lao kama Taasisi ya mikopo ya next generation kuwa na moyo ya kusaidiana wenyewe na kutatua changamoto zilipo katika jamii yetu.
Mbali na hayo ametoa rai kwa makampuni na taasisi mbalimbali kutambua nafasi zao na umuhimu wa michango yao mbalimbali katika kuisaidia serikali kutatua changamoto zinazoikabili jamii na Taifa kwa ujumla.
Hata hivyo Kansapa amewataka vijana kujitenga na makindi ya kiharifu , matumizi mabaya ya utandawazi na kuelekeza juhudi zetu katika maendeleo ya nchi yetu.
Kwa upande wake Katibu wa chama cha watu wasioona Billy Mbawa amesema siyo serikali pekee inayoweza kusaidia walemavu hata Taasisi zinajukumu la kusaidia watu wenye uhitaji ili kufikia malengo yao nakuleta maendeleo katika nchini.
Taasisi ya next generation Microfinance inayojihusisha na utoaji wa mikopo kwa kada mbalimbali ikiwemo watumishi wa umma ,watumishi wa sekta binafsi , wafanyabiashara na wajasiriamali wakiwemo walemavu.
Next generation Microfinance mpaka sasa wameweza kutoa mikopo kwa watumishi 278 , wafanyabiashara 125 pamoja na vikundi vya wajasiriamali vipatavyo 27 sambamba na vijana kujiajiri kupitia mikopo yao.