- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NECTA YAPUNGUZA IDADI YA MASWALI MTIHANI DARASA LA 7
Baraza la mitihani limetangaza kuanza kwa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi kuanzia leo jumatano huku wakifanya mabadiliko katika mfumo ,wakipunguza baadhi ya maswali kutoka hamsini mpaka arobaini na tano.
Mtihani huo utakaohusisha wanafunzi wapatao 960,202
Akizungumza kuhusiana na mfumo huo ambapo kwa sasa kutakuwa na maswali matano ya kujieleza tofauti na awali ambapo maswali yote yalikuwa ya kuchagua katibu mtendaji wa baraza hilo Dkt.Charles Msonde amesema hiyo ni katika kuboresha zaidi.
Pia Dkt. Msonde amezitaka kamati za mitihani za mikoa, halmashauri, na manispaa kuhakikisha taratibu zote zinazingatiwa za usalama na amani pamoja na kuhakikisha udanganyifu unadhibitiwa. ITV imepita katika shule mbalimbali na kukuta wanafunzi wakiwa katika maandalizi ya mwisho kuelekea mtihani huo