- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NEC YATANGAZA SIKU NA TAREHE RASMI YA UCHAGUZI WA MARUDIO
Dar es Salaam: Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza rasmi kuwa Desemba 2, 2018 itakuwa ni uchanguzi mdogo wa ubunge katika majimbo ya Simanjiro, Serengeti na kata 21 za Tanzania Bara zilizoachwa wazi na wabunge Waliohamia chama tawala CCM.
Kwamujubu wa Taarifa iliyotolewa leo Oktoba 15, 2018 na kitengo cha mawasiliano cha NEC kimemnukuu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Semistocles Kaijage akisema fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kati ya Oktoba 28 hadi 03 Novemba, 2018.
“Uteuzi wa wagombea utafanyika Novemba 3, 2018. Kampeni za uchaguzi zitafanyika kuanzia Novemba 4 hadi Desemba 1 mwaka huu na siku ya uchaguzi itakuwa ni Desemba 2, 2018,” amesema Jaji Kaijage
Mwenyekiti huyo amesema Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, aliitaarifu tume uwapo wa nafasi ya ubunge katika majimbo hayo.
Jaji Kaijage amesema barua hiyo imepokelewa kufuatia wabunge wa majimbo hayo Marwa Ryoba Chacha na James Millya kujiuzulu na kutoka kwenye vyama vyao vya Chadema na kuhamia CCM.
Amesema tume pia imepokea taarifa kutoka kwa waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa ambaye kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, aliitaarifu tume uwapo wa nafasi za madiwani katika kata 21 za Tanzania Bara. Nafasi hizo zimetokana na sababu mbalimbali ikiwamo vifo na kujiuzulu.
“Tunapenda kuvikumbusha vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia Sheria, Kanuni, Maadili ya Uchaguzi, Taratibu, Miongozo na maelekezo yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa kipindi chote cha Uchaguzi huu mdogo,” amesema.