Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 11:45 pm

NEWS: NDUGAI AWATAKA WABUNGE KUTAMBUA NAFASI ZAO KATIKA JAMII.

DODOMA: Spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai amewataka wabunge kuzingatia maadili na miiko ya uongozi wawapo ndani na nje ya bunge kwa kutambua nafasi yao katika jamii hali itakayosaidia kutofumbia macho vitendo vya rushwa na ufisadi.

Kanuni za maadili na kanuni za maadili ya utendaji ni nyenzo muhimu katika mapambano dhidi ya rushwa na kuzuia tabia zisizo za kimaadili ambapo wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi katika maeneo yao wametakiwa kuwa mfano wa kuigwa katika kuzingatia maadili na miiko yauongozi

Akizungumza na wabunge ambao ni wajumbe wa Chama cha wabunge wanaopambana na Rushwa APNAC spika wa bunge Job Ndugai amesema kuwa ili kukabiliana na vitendo vya rushwa na ufisadi ni vyema wabunge wakazingatia kanuni na maadili ya uongozi


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha wabunge wanaopambana na Rushwa APNAC ambaye pia ni mbunge wa Karatu Cesilia Pareso amesema kuwa viongozi wanawajibika kuisimamia serikali katika kupinga na kudhibiti vitendo vya rushwa na ufisadi


Baadhi ya wabunge ambao ni wajumbe wa Chama cha wabunge wanaopambana na Rushwa APNAC wamesema kuwa kupitia mtandao huo umekuwa chachu ya mapambano dhidi ya rushwa huku wakitaka nguvu iongozwe ili kuondoa rushwa nchini


Mnamo mwaka 2003 mkataba wa umoja wa mataifa wa mapambano dhidi ya rushwa ulijumuisha kanuni za maadili ya utumishi wa umma kama kipengele muhimu katika kuzuia mgongano wa maslahi na rushwa