- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NDUGAI AITOLEA UVIVU WIZARA YA TAMISEMI
Dodoma: Spika wa bunge la Jamhuri wa muunga wa tanzania na Mbunge wa Kongwa mkoani Dodoma Job Ndugai ameoneshwa kusikitishwa na kitendo cha Wizara ya Tamisemi kuwapangia vituo vya kazi walimu wapya na kuhoji kwa nini kazi hiyo wamezipokonya halimashauri hapa nchini.
kauli hiyo ameitoa leo Juma mosi Decemba 23, 2017 baada ya Jana Waziri wa TAMISEMI Bw. Slemani Jaffo kuwapangia walimu wapya 3,033 vituo vya kazi, spika amesema kuwa TAMISEMA imekuwa ikirudika walimu kwenye shule zisizo na mahitaji ya walimu.
"Hili jambo linakera kila mahali sasa ni Tamisemi, hadi napata shaka sasa, hivi hii dhana ya D by D (Uugatuaji madara) inamaana haijatafsiriwa vyema au ndio kupoka madaraka kutoka kwa wengine," alihoji Ndugai
Spika alijaribu kutolea mfano shule ya Banyibanyi iliyopo kongwa ambayo inawanafunzi wa kidato cha Tatu lakini hawajawahi kusoma masomo ya sayansi hata siku moja
"lakini juzi hapa mmepanga walimu na nilipita kwa mara nyingine tena lakini hakuna mwalimu hata mmoja na hawajasoma masomo ya fizikia, baiolojia na kemia, nauliza tena hivi hawa Tamisemi walisoma shule gani na ninyi mmesoma wapi" aliuliza Ndugai