- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NDOA ZA UTOTONI BADO NI JANGA NCHINI.
DODOMA: Ndoa za utotoni zinazosababishwa na sababu mbalimbali zikiwemo mfumo dume,ukandamizaji wa kitabaka,umri pamoja na sababu za kiuchumi unatajwa kuwa kikwazo cha maendeleo ya mtoto wa kike nchini Tanzaniana .
Hayo yalibainishwa jana na wanahabari mkoni hapa wakati wa mjadala maalumu kuhusu sababu zinazopelekea mimba za utotoni nakupelekea ndoa za mapema na kudidimiza ndoto za wasichana.
Akizungumza kwa niaba ya wanahabari wengine katika mdahalo huo uliodhaminiwa na chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA) Mussa Enock amesema sababu za kiuchumi na ukandamizaji zilizopo katika jamii zinamkandamiza mtoto wa kike na kushindwa kufikia malengo.
Kwa upande wake Rahel Chibwete amezitaja baadhi ya sababu zinazosababisha mimba na ndoa za utotoni kuwa ni pamoja na uhaba wa maji,umbali wa shule,umaskinina utandawazi.
Hata hivyo ameongeza kuwa sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inayoruhusu ndoa kwa ridhaa ya wazazi ni kikwazo ambacho hakifai kuendekezwa na kuitaka serikali kuiangalia upya.
“Umbali wa shule ni kikwazo kwa watoto wa kike kwa kuwa huwalazimu kushawishika kujihusisha katika mahusiano ya mapenzi na waendesha pikipiki katika umri mdogo ili kurahisisha suala la usafiri,”amesema Chibwete.
Akiongea kwa niaba ya TAMWA ,afisa taarifa na miradi Leonida Kanyuma amesema, katika kuhakikisha mtoto wa kike analindwa,chama hicho kimeanzisha mradiili kuchangia kuboresha maisha ya mtoto wa Tanzania kwa kupigania usawa wa jinsia na uwezeshaji kwa kuweka jicho la jinsia ndani ya siasa.
Mbali na hayo Kanyuma amesema mradi huo unalenga zaidi kupunguza ukatili wa kijinsia na ikiwezekana kuutokomeza kabisa ikiwa ni pamoja na kuboresha uwezowa kiuchumi kwa wanawake na kujenga uelewa kwa vyombo mbali mbali katika kuwalinda wasichana kutokana na mimba za utotoni na kuolewa mapema..
Mwanaharakati huyu hakusita kutaja madhara ya mimba za utotoni kuwa ni pamoja na kuathiri suala zima la elimu na kupunguza ari ya watotowengine kuendelea kusoma ikiwa ni pamoja na kuathirika kisaikolojia.
Mbali na hayo amesisitiza kuwa kila mwanajamii anapaswa kuishi kwa amani ikiwa ni pamoja na kuwa makini kuripoti matukio ya ukatili yanayolenga kuwarubuni watoto wa kike kwa vyombo husika ili kuweza kuwawajibisha wahusika.