- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NDALICHAKO ATAJA SIFA ZA UOMBAJI WA MKOPO WA ELIMU YA JUU.
DODOMA: Waziri wa elimu,sayansi na technolojia Joyce Ndalichako amesema katika kuhakikisha wakati wa kuwasilisha maombi ya mkopo wa elimu ya juu , mwombaji kuawasilisha taarifa muhimu zikiwemo shuleau vyuo alivyosoma kabla ya kujiunga na elimu ya juu.
Akijibu swali la mbunge wa Mbozi Paschal Haonga aliyetaka kujua ‘Je, bodi ya mkopo haioni kama kuna baadhi ya wanafunzi hulipiwa ada ya shule za binafsi na ndugu, jamaa na NGO’s hivyo wanafunzi wanapofikia elimu ya juu kushindwa kumudu gharama za elimu ya juu’.
Ndalichako amesema sifa za msingi za kupata mkopo wa elimu ya juu zinaainishwa katika kifungu cha 17 cha sheria ya bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (sura 178).
Akifafanua zaidi amesema mwombaji awe mtanzania, awe amedahiliwa kwenye chuo kinachotambulika, awe ameomba mkopo kwa njia ya mtandao (OLAMS)na awe hana chanzokingine cha kugharamia elimu yake.
Mbali na sheria vingizo vingine ni uyatima,ulemavu, uhitaji na mahitaji ya rasilimali watu kwa ajili ya vipaumbele vya maendeleo vya taifa.
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka wa masomo wa mwaka 2016/17 , jumla ya wanafunzi 719 waliothibitika kufadhiliwa au kusaidiwa katika masomo yao ya sekondari walipata mikopo