Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 11:46 am

NEWS: NCHI ZA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI ZASHIRIKIANA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA WA MATAIFA YAO.

DODOMA : Katika kuendelea kudumisha amani,ulinzi na usalama ukanda wa Afrika ya mashariki na nchi za ukanda wa SADC Jeshi la wananchi wa Tanzania limesema kuwa kuwapo kwa ushirikiano wa kiuchumi kwa mataifa hayo kunasaidia kuimarisha ulinzi kwa nchi hizo na kuziondolea hofu ya kushambuliana zenyewe kwa zenyewe.

Tanzania imekuwa ikishirikiana na mataifa mbalimbali katika shughuli za maendeleo lakini pia imekuwa ikishirikiana na majeshi ya ulinzi na usalama kwa mataifa mbalimbali katika kulinda amani na kuzuia uhalifu na kusaidiana katika sekta za ulinzi na nchi za afrika mashariki na sadc kunaepusha nchi hizo kutoshambuliana.

Kanali Sweetbert Ruta wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ambaye amewaongoza maafisa na wanafunzi 32 kutoka chuo cha mafunzo ya kijeshi Duruti mkoani Arusha ambao wametembelea kiwanda cha magodoro cha Dodoma Asili, amesema uchumi unaanzia kwenye amani na bila kuwapo na amani hakuna uchumi


Aidha katika hatua nyingine Kanali Sweetbert Ruto amesema kuwa jeshi la wananchi Tanzania litaendelea kushirikiana na majeshi mengine katika kusimamia ulinzi na usalama wa mataifa hayo


Naye Luteni Kanali Peter Kimondiu wa Jeshi la Kenya ambaye ni mkufunzi wa chuo cha kijeshi Duruti, amesema wamefanikiwa kuwatembeza wanafunzi wanaochukua mafunzo chuoni hapo kwa lengo la kujifunza na kuona uchumi wa Tanzania


Afisa usajili wa kiwanda cha magodoro cha dodoma asili, Emily Sagala, amesema maafisa hao wameweza kuona jinsi viwanda vya Tanzania vinavyoweza kuzalisha vitu vyenye ubora zaidi.

Ziara hiyo ina lengo la kujifunza maswala mbalimbali ikiwemo ya kiuchumi ambapo kwa sasa Tanzania imekuwa ni miongoni mwa nchi zinazoelekea uchumi wa viwanda ifikapo 2020