- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : NATO WATAHADHALISHA KUHUSU VITA YA KOREA KASKAZINI
Katibu Mkuu wa Nato atahadharisha kuhusu vita na Korea ya Kaskazini
Katibu Mkuu wa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) amezitahadharisha nchi zote husika kuhusu kupigana vita na Korea ya Kaskazini.
Jens Stoltenberg ambaye yupo ziarani nchini Japan amesema kuwa, vita na Korea ya Kaskazini ni suala ambalo litaitumbukiza dunia katika msiba na maafa. Stoltenberg amesisitiza kuwa, hakuna nchi yoyote mwanachama wa Nato inayetaka kushuhudia mapigano yakijiri na Korea ya Kaskazini na kwamba nchi hizo zinaamini kuwa, vita hivyo vitasababisha maafa makubwa.
Katibu Mkuu wa Nato (kushoto) akisalimiana na Shinzo Abe Waziri Mkuu wa Japan hukoTokyo
Wakati huo huo Katibu Mkuu wa NATO ameunga mkono misimamo ya Korea ya Kusini na Japan kuhusu kadhia ya Korea ya Kaskazini na kueleza kuwa, nchi nyingine wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikiwemo Russia, zinaweza kutafuta njia za amani za kuutatua mgogoro wa Peninsula ya Korea.
Matamshi hayo ya Jens Stoltenberg yametolewa huku mivutano kati ya Marekani na Korea ya Kaskazini ikipambana moto ambapo Rais Donald Trump ameonekana mara kadhaa akitumia lugha ya vitisho ya kutaka kuishambulia kijeshi nchi hiyo. Pyongyang nayo imejibu vitisho hivyo vya Trump ikisisitiza kuwa, itaendelea kuimarisha nguvu zake za kiulinzi madhali Marekani na waitifaki wake wanaendeleza harakati zao za kijeshi na kutoa vitisho dhidi ya Korea ya Kaskazini.