Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 4:39 pm

NEWS: NASSARI ALMANUSURA AWAWE NA WATU WASIO JULIKANA

Arusha: Mbubge wa Arumeru mashariki Joshua Nassari amevamia nyumbani kwake maeneo ya Usa river wilaya ya Arumeru mkoani Arusha usiku wa kuamkia leo, akituo taarifa kupitia ukurasa wake wa twitter Nassar amesema kuwa amefanikiwa kukimbia yeye na mke wake nyumbani kwake usiku baada ya kuvamiwa na watu wenye silaha na wamefanikiwa kuwaua mbwa wake wawili waliokuwa wanalinda nyumabni kwake.

"Nimevamiwa nyumbani kwangu maeneo ya USA RIVER usiku huu na watu wenye silaha, na kufyatua risasi ambazo zimeua mbwa waliokuwepo nje ya nyumba. Nimefanikiwa kukimbia na mke wangu na kuripoti kituo cha Polisi. Nimekuwa nikitishiwa kuuawa kila siku, sina amani ndani ya nchi yangu" aliongea Nassari

Kwa upande wake Mbunge wa Tarime mjini John Heche amelaani kitendo hicho na kuona ni kitendo kiovu na kinapaswa kikemewe na kila mtanzania "Hii ni njia ovu ya kujaribu kumtia hofu kila mtu. Ni wazi sasa kwamba usalama wetu uko shakani sana. Lazima hali hii ikemewe na kila Mtanzania mpenda haki. Pole Nasari lazima tutavuka. alisema Heche

Polisi wamefika nyumbani kwa Mbunge Nassari na kuanza uchunguzi wa shambulizi hilo la risasi na watatoa taarifa baadae